VIDONDA VYA TUMBO

  
PEPTIC ULCERS almaarufu kama Vidonda Vya Tumbo hutokea hasa pale ambapo mtu hana kitu kinachoepusha acid iliyomo ndani ya tumbo kutafuna kuta za tumbo lake. Ulcers hutokea si kwenye tumbo tu, bali pia na katika mwanzo wa utumbo mdogo (Duodenum) na hivyo kuitwa Duodenal Ulcers.

JINSI ULCERS INAVYOTOKEA

Ndani ya tumbo lako, kuna substances vinavyopatikana ndani ya tumbo navyo hujulikana kwa majina Hydrochloric Acid (HCl) na Pepsin Enzyme. Hizi mbili hutumika katika kumeng’enya chakula kilichomo tumboni lakini ukosefu wa chakula ndani ya tumbo lako hupelekea substances hizi kujijenga kwa haraka na kuanza kuharibu mistari iliyoko ndani ya tumbo ama Gastrointestinal-GI Tract.

Ulapo chakula acid hiyo ambayo huwa katika ukali unaoendana na hali ya tumbo lako husafishwa na chakula hicho lakini kwa wakati mfupi na ikitumika kama kivunjio cha virutubisho vinavyopatikana kwenye chakula.

Acid hii hurudi mara kwa mara ili kuendelea kutafuta chakula cha kumeng’enya kupata virutubisho vihitajiwavyo na mwili na chakula hicho kinapokosekana ndipo pale ambapo acid inamwagika katika kuta za tumbo na hivyo kupelekea vidonda kutokea. Hali ya vidonda hivi kuwemo ndani ya tumbo na urudiaji wa kumwagika kwa acid hii huchokoza vidonda hivi na hivyo kuvitonesha na kukupelekea kusikia uvimbeuchungu au moto ndani ya tumbo au zaidi maumivu makali.

Utafiti umesema kuwa zaidi ya wagonjwa 35% wenye ulcers hupatwa na matatizo mengine ambayo mengi huweza kuzuilika. Wachache hupatwa na Perforation of the Lining GI (Gastrointestinal) Tract (kitobo katika kuta za mistari ya tumbo) na kuvuja kwa damu ndani kwa ndani.

VISABABISHI VIKUU

Vidonda vya Tumbo husababishwa mara kwa mara na mambo tofauti ambayo hatuna budi sisi wanadamu kuwa nayo. Uchunguzi uliofanywa miaka ya 1980 nchini Marekani ulisimamia kwamba Ulcers za aina yeyote ile husababishwa sana na mtu kuwa na stress ya kupindukia. 

Lakini uchunguzi huu ulikanushwa miaka hii ya hivi karibuni na Madaktari huku  wakisema kwamba Ulcers husababishwa na mambo yafuatayo;

1.Msongo mkubwa wa Mawazo

2.Utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya Anti Inflamatory Drugs(NSAIDs kama Aspirin)

3.Mfumo mbovu wa Maisha (Poor Lifestyle)

4.Maambukizi ya Bacteria. Maambukizi haya husababishwa na bacteria Helicobacter pylori - H. pylori wanaosambazwa na maji

DALILI ZA ULCERS

Hatuwezi kukimbilia kuelezana jinsi ya kuua ulcers ulizonazo bila ya kuelezena dalili zake. Kwa wengi ulcers haziumizi tu bali pia huweza kuleta matatizo kama maradhi, kubadilika kwa ladha mdomoni, kutapika n.k. Unataka kujua jinsi ulcers zianzavyo, zifuatazo ni dalili kuu zinazosababishwa na ulcers;

1.    Maumivu sehemu ya kiuno (baada ya kula) na Kichomi (sehemu kati ya tumbo na kifua)
2.   Kutapika damu au kukojoa damu au kinyesi chenye damu
3.   Nausea na  Kutapika
4.   Kinyesi kuwa cheusi
5.   Kukosa hamu ya kula na kupungu uzito
6.   Kukosa usingizi kwa sababu ya maumivu makali usiku
7.   Tumbo kujaa gesi
8.   Upungufu wa maji mwilini na kuishiwa na nguvu.

JINSI YA KUPUNGUZA NA KUUA VIDONDA VYA TUMBO

Nadhani hadi tulipofikia, inafaa sasa kuelezana jinsi ya kuua vidonda vya tumbo. Njia zote ni rahisi hasa kama utazingatia mwenendo wa lifestyle yako wewe mwenyewe:

1.   Punguza kuwa na msongo wa mawazo (reduce overstressing).

Siku moja imetokea kwamba umepatwa na tatizo moja la kuondokewa na kitu au mtu umpendaye kwa dhati, ni kawaida kwetu sisi wanadamu kuwakumbuka tuliopotelewa nao lakini ni hali ya kila mwanadamu kupotelewa na kitu aghalabu mtu maishani mwake. Jambo hili lisiwe gheni kwako kwa kuwa utakuwa ndani ya mateso yako wewe mwenyewe.

Unapokuwa na msongo wa mawazo ni dhahiri kwamba unatoa nafasi kwa ulcers kuingia katika maisha yako. Upotewapo na mtu, huna budi kuwa katika hali ya mawazo, kufukuzwa kazi pia utakuwa katika hali hiyo hiyo au mpenzi wako unayempenda kupitiliza akakutema ndiyo hapo utakapotamani dunia ipasuke na kukumeza. Yaache yaliyopita yawe yamepita.

Uchunguzi umesema kuwa msongo wa mawazo humfanya mgonjwa wa ulcers kuyakaribisha maumivu makali ndani ya maisha yake kwa kuwa mfumo wa kumeng’enya chakula (Digestive system) unauhusiano wa moja kwa moja na ufanyakazi wa ubongo (Gut-Brain Connection).

Mwili hutuma signals za uwoga, hofu, huzuni, msongo wa mawazo, kukosa raha na hata depression (sonona) kwenda kwenye ubongo hivyo kuyapa magonjwa tajwa mwanzo nafasi.

IIi kuweza kuendesha mawazo yako, tazama Jinsi ya kuzuia msongo wa mawazo au tumia dawa asilia za kuzuia msongo wa mawazo kama kufanya mazoezi mara kwa mara, meditating, kusali, kutembea kila jioni sehemu mbalimbali jijini kwako, kupata usiingizi wa kutosha n.k.

2.  Punguza matumizi ya Dawa za kutuliza maumivu (NSAID Pain Relievers)

NSAID Pain Relievers (Non-Steroidal Anti-Inflammatory Medications) ni dawa zinazojulikana kupunguza maumivu kwa haraka sana pale zinapotumiwa na mgonjwa.  Dawa hizi hutuliza maumivu ya kichwa, homa kali na uvimbe lakini haziponyi mara, sana sana ni kama kitulizo tu. 


Watu wengi huzitumia mara kwa mara bila ya kujua kwamba zinamadhara wakitegemea kwamba zitawasaidia moja kwa moja.

Kiujumla dawa hizi husababisha magonjwa mengine yawe sugu ndani ya mwili wa mtu kwa sababu magonjwa hayo yatakuwa na tabia ya kujirudia mara kwa mara. Maumivu huwa makali hasa pale ambapo gonjwa limejirudia kwa mara ya tatu kama Kuumwa na kichwa (headache), maumivu ya viungo vya mwili (joints of the body), misuli kukaza (muscle cramps), misuli kuchanika (muscle tearing), homa (fever), na kadhalika.

Ushauri umetolewa kwamba mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo asitegemee sana dawa za kupunguza maumivu kwani ufanyaji kazi wa akili huwa na uhusiano wa moja kwa moja na tumbo. Utafiti umesema kwamba mtu huyu atajisababishia vidonda kwenye kuta za tumbo na hivyo kujiweka hatarini na maumivu makali zaidi.

Ninukuu kutokusema kwamba usizitumie dawa hizi bali ninukuu kusema kwamba usizitegemee sana. Kupunguza kutumia dawa hizi husaidia kuepusha utengenezaji wa acidi inayochoma vidonda ndani ya tumbo. Zitumie dawa hizi kulingana na ushauri wa daktari kwa muda aliokushauri uzitumie. Usizidishe hata kama umeona hujapona, utajizidishia maradhi.

3.  Tafuta tiba mbadala

Nenda hospitali ukapate matibabu kamilifu yanayoweza kukupa njia ya kuepukana na uvimbeuchungu (Inflammations) zinazosababishwa na H. pylori ambaye huumiza tumbo na utumbo mdogo kwa kuutafuna na kutengeneza mikato ambayo ni migumu kupona. Huweza kusababisha pia kuvuja damu kwa ndani.

Helicobacter pylori huharibu kamasi (mucous coating) linalopatikana kwenye mistari ya tumbo na mwanzo wa utumbo mdogo na hivyo kuchangia kukuza idadi ya vidonda ndani ya tumbo na hivyo kuzidisha maumivu. H. pylori husambazwa kwa njia ya maji taka na machafu, chakula kisichopikwa vyema, au vifaa vichafu vya kulia.

Ongeza kinga ya mwili kwa kuachana na mwenendo mbovu wa maisha yako nikimaanisha namna ya kuishi wewe kama wewe. Pia kuachana na tabia mbaya kama uvutaji wa sigara (smoking), ulevi na kuwa katika sehemu zenye kemikali zinazoharibu mwili (toxic exposure). Usitumie vyakula vya kutengenezwa (processed food), sio vizuri.

Hivyo kama unavyo vidonda vya tumbo ni vyema ukaenda hospitali kupata matibabu kama tayari ulishajihusisha na tabia tajwa hapo juu.  Usiwe mwoga wa sindano. Jikaze, nenda hospitali.

4.  Kula lishe bora na achana na Processed foods.

Ushazoea chipsi, mahanjumati ya kununuliwa supermarket, basi utafiti unasema ni afadhali kula chipsi zilizotengenezwa ukiona pale mjini – ingawa haishauriwi kuliko kula vyakula vya kutengeneza kama nyama, nyanya, matunda kama apples, mboga za majani kama kabichi za kutengeneza n.k huongeza vidonda vya tumbo kwa kuwa havimengenywi ipaswavyo na hukosa virutubisho vyote muhimu.

Ukiachana na hilo, kuna lile tulilozoea wengi wetu kwamba kuna kuruka mlo mmoja wa siku hasa ule wa mchana. Basi tambua kwamba kula chakula mara mbili – asubuhi na jioni – kwa siku na kuruka mlo mmoja hasa wa mchana huongeza kwa kasi kubwa idadi ya vidonda ndani ya tumbo kwa hiyo usijidanganye kula chakula kilicho shiba asubuhi na jioni ndio kwamba unazuia kupata vidonda vya tumbo.

Kulingana na Jackson Seigelbaum Gastroenterology Center, vyakula ambavyo hutoa hali nzuri ya tumbo kufanya kazi kawaida huhusisha;

i.      Vinywaji vyenye Caffeine
ii.    Pilipili manga (red/hot pepper) na chili powder
iii.   Kahawa kali (decaffeinated coffee/tea)
iv.   Pombe na vilevi
v.    Cocoa, chocolate na vinywaji vyenye cola
vi.   Limau, ndimu n.k na juisi zake (citrus fruits)
vii.  Black pepper

Jitahidi kuepukana na vyakula vya namna hii na jihusishe zaidi na lishe iliiyobora yenye mboga mboga zisizo za kutengeneza, nyama kutoka buchani sio dukani, na chakula kilichopikwa vyema kabisa au kula lishe ya mediterani (Mediterranean diet).

Kama ulcers zako husababisha kutapika na kichefuchefu, ni vyema sana ukaepusha kupungukiwa na maji mwilini (dehydration), electrolyte imbalances na upungufu wa madini hitajika mwilini (nutrient deficiencies).

USHAURI MWINGINE JUU YA KUENDESHA LISHE YAKO;

i. Jitahidi kuwa na uzito utakaoshauriwa na daktari na zuia unene wa kupindukia (obesity).
ii.   Epusha unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara
iii.  Epusha vya moto sana
iv.  Kula vyakula vidogo vidogo katikati ya siku

Hivyo ndivyo utakavyoweza kupunguza kuwa na maumivu makali ya sehemu usiyoweza kuishika na wala hushauriwi kujaribu kupachokoza hapo kwa kuwa ni kati ya sehemu nyeti sana za mwili wako ambazo huweza kukusababishia kifo mara tu utakapopatibua.

Tuambie, unafikiri nini juu ya mada hii! 

Comments