JINSI
YA KUFAULU MASOMO YA SCIENCE NA MATHEMATICS.
Mwanafunzi hana budi kutambua kwamba wanadamu
tunaelekea ulimwengu wa aina gani. Sayansi ni kati ya sehemu inayojenga
ulimwengu huo na kwetu sisi Watanzania, hatuna budi kuipenda sayansi inayokuwa
kwa kasi.
Ugunduzi wa mambo mbalimbali ndiyo unaohitajika kwa sasa ili kuifanya
nchi yetu ifikie nafasi tunayoitafuta 2nd World Country.
Wanafunzi tulio wengi husema kwamba Sayansi ni ngumu kuliko Arts na Biashara lakini ndani ya mioyo yetu tunatambua kwamba sio kweli.
Kama huamini muuluze mwanafunzi mwenzako kati ya kuweka matukio
yaliyopita yaliyofanyika hapo zamani kichwani mwakona kufanya hesabu juu ya
Moles za Liquid H na kupiga Hesabu ya Jinsi ya kupata umbali kutoka Point A
kwenda Point B Kati ya sababu zinazopelekea tukajiwekea fikra za namna hiyo ni
kwamba;
01. Si rahisi kuonekana.
Nikimaanisha kwamba si rahisi kwa sisi
kuyaona yanayozungumziwa na yanayosemwa. Kwa kawaida huitwa Kusadikika kwa
sababu ni THEORY. Hatuna budi tukiwa na lengo la kufauli masomo haya,
Kuyaangalia kwa jicho la tatu.
02. Ni vigumu kuelezea.
Ni ngumu kuiweka wazi hasa kwa walimu
wasio wazoefu na masomo yenyewe. Simaanishi hawajui, bali hawana uwezo
wakuorodhesha wanayofundisha kwa wanafunzi, hivyo ni vigumu kwa wanafunzi kusema
tumeelewa kutoka moyoni. Mwalimu anahitaji kulijua somo analofundisha kutoka
moyoni ili aweze kuwaimarishia wanafunzi msingi wa kuyapenda masomo hayo.
03. Upeo wa CALCULATIONS!
Calculate(Kokotoa)!!! Ni neno rahisi
sana lakini ni zito kuliweka kwa vitendo. Hii ni kwa sababu ni kuhesabu.
Kucheza na namba, ndiyo maana kuu ya neon hilo, "Finding X and Y"
ndiyo mada kuu ya masomo haya na ndiyo maana watu wanashindwa kujiweka wazi
kukubali kuwatafuta watu hawa wawili. Ukiweza kucheza na namba, utaweza kucheza
na masomo haya yote lakini si rahisi kihivyo.
Hivyo basi, Tufanye nini?
Hizi ni mbinu chache ambazo mimi mwenyewe na kwa usaidizi kutoka kwa wakali wenzangu wa masomo haya wanazozitumia kufaulu masomo haya:
01. Kukumbuka rules, laws, na equations kwa kuelewa umuhimu wake.
Kukumbuka ni kitu kimoja na kuelewa ni kitu kingine lakini chenye
uhusiano mtimilifu na unachokumbuka. Hivyo, kama unaweza kuelewa
F=mg
(F-force;
m-mass, g-gravity)
Formula hii ya NEWTON basi ni rahisi sana kuikumbuka tena bila
matatizo. Hii inachangiwa pia na ufupi wake, lakini ukipewa TRIGONOMETRY
‘Identity 1’
Sin (A+B) = SinACosB +/- SinBCosA
Ninauhakika kwamba kuna wengi watakao changanyikiwa na wasijue cha
kufanya. Hii ni kwa sababu watashindwa kuikumbuka kwenye mtihani na hata kama
wataweza basi hawataweza kujua waanzie wapi kama hawatapewa vitatu au vinne
kwenye swali hilo na kama wataichanganya na Trig ‘Identity 2'
Cos (A+B) = SinASinB +/- CosACosB
Tuliza akili, iangalie formula na usiiogope wala kupanic kwa sababu iko tu kwenye maandishi kisha ifananishe na vile unavyoelewa wewe kisha ijaribu, Nakuhakikishia kwamba ni wazi kabisa kwamba utapata swali kwa asilimia 70% au 85%.
02. Don't Give Up.
Kwa njia yeyote ile, hata kama hujawahi kufundishwa nina uhakika
kwamba kujaribu kwako kwa swali lililo mbele yako bila kuogopa kutakupa nafasi
nzuri ya kuweza kulitatua swali litakalofuata na kwa asilimia kubwa ukaweza
kulipata. kwa nini umeliweza? ni kwa sababu hujakubali kushindwa na kitu
kilichowekwa kwako.
QN: What point will become zero velocity at a thrown up
object?
ANS: The point that the
object will be at zero velocity is when the object is at the maximum point on
the air without contact before it begins to fall back.
Jaribu hili, tena ni rahisi sana,
QNs:
- Why does the sky happen to appear blue and not red?
- Why does the Earth revolve around the Sun but does not
revolve towards it?
03. Know the basics (Jua yote uliyoanza kufundishwa.)
Tukija kuangalia MATHS, tunaona kwamba FORM-III kwenye Sub-topic ya COMPOUND INTEREST, ukitaka swali liishe kiurahisi bila ya wewe kuanza kuzidisha namba moja-moja, unahitaji kutumia LOGARITHMS ambayo ni topic ipatikanayo FORM-II tena bila shida utaweza kulifanya swali hilo. Huo ni mfano mmoja tu.
Ukishindwa kuelewa topic ya MOLE CONCEPT ya
FORM-III: CHEMISTRY, ni wazi kabisa hutaweza maswali kadha wa kadha ya Mtihani
wa mwisho FORM-IV NECTA.
Hivy basi, jitahidi kwa kadri uwezavyo kuzielewa topic zote ambazo
ulisha kwisha zipitia vidato vya nyuma ili uweze kuyaweza masomo ambayo tofauti
kabisa na masomo mengine.
04. Maneno ya
Wengi(What People say).
Wanafunzi wengi naamini kwamba tumekuwa tukisikia maneno ya
waliopita kuwa MATHS ni ugonjwa wa taifa, wengine
husema Topic ya CIRCLE, NA SPHERE ni ngumu sana na
wengine husema PHYSICS inachanganya lakini si kweli.
Kwani walio weza kufundisha Maengineer wa nchi hii, Marubani kama William Zelothe Stephen anaye endesha AIRBUS
A319 na Madaktari wao wameweza vipi?
Usisikilize yaliyokwisha kusemwa kwa sababu yatakurudisha nyuma
katika maendeleo yako. Shule niliyopo mimi wanafunzi waliopita FORM-IV walikuwa
wakisema ACCOUNTS ni topic ngumu sana lakini nilikuja
kugundua na class-mates wenzangu kwamba wale walikuwa wakipata maneno kutoka
nje kwamba topic hiyo ilikuwa ngumu, na mpaka sasa, topic hiyo ndiyo inayotupa
marks za kutosha.
Usisikilize watu wanaovunja moyo na sana pendelea kukaa na watu
unao dhani kwamba kabisa watakusaidia kufaulu.
05. Take your
Time (Muda na Utayari).

Kwa mfano, Albert Einstein aliweza kuhakikisha kwamba Brownian
motion ni kweli kwa kuweka chembechembe ndogo kwenye maji na kutengeneza Zigzag
motion.

Kama watu hawa wawili-Albert
Einstein(1879-1955) na Robert Brown(1773-1858)- waliweza kuchukua mda
kugundua na keweka wazi vitu hivi basi hata wewe waweza kutumia mifano hii
katika kujiandaa kwa kusoma na kuyapenda masomo haya ili uweze kupataufaulu
mzuri wa masomo haya.
06. Yapende
Masomo
Kama kweli ungependa kuyafaulu haya masomo basi yapende. Najua hii
itakuwa vigumu sana kukubaliana nayo hasa tukizingatia kwamba wengi wetu ni
wapenzi wa ARTS (i.e Music, Movies etc).
Lakini hata kama unapenda hizi arts, basi sio kwamba huwezi
kupenda na SCIENCE. Nilikuwa kati ya top 10 waliokuwa wakifeli Physics na
nilikuwa mpenzi wa kuwatch movies. nilitokea kuanza kufaulu PHYSICS baada ya
kuja kukutana na TV show iitwayo THE FLASH kutoka DC Int.
Filamu hii imekuwa sababu kuu ya mimi kupenda Physics na
Maths kwa sababu yenyewe inaenda sambamba na robo ya Topics nilizofundishwa
tokea FORM-I hadi sasa na hata zingine kunipelekea nizijue na kunisaidia kujibu
maswali ambayo kiukweli bila ya ufahamu wake nisingeyaweza. Tokea hapo niliweza
kumshawishi mwalimu wangu kuweka NIKE (√) kwenye jibu langu kwa njia zangu
zinazozidi hata njia alizofundisha yeye. Si kila Filamu inapotosha!
MWISHO, FINALLY.......................
Uwezo wako wewe wa kuweza kujibu mitihani ya PHYSICS, MATHEMATICS
na CHEMISTRY hata BIOLOGY na GEOGRAPHY uko sasa mikononi mwako. unataka
kufaulu, basi kuwatayari kufaulu ni maamuzi yako wewe mwenyewe kwa sababu
hakuna atakayekutengenezea maisha yako ya baadaye bali watakusaidia tu
kukuonyesha kwa kwenda na kufanya lakini sio kufanya.
So what are you waiting
for? Kick the Cs, Ds and Fs to hell and take up your rightful place to the Bs
and As. That's where you belong!!!
Tafadhali weka comment juu ya jambo hili. utakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wote watakao soma hapa.
Tafadhali weka comment juu ya jambo hili. utakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wote watakao soma hapa.
Comments
Im from juhudi high school