JINSI YA KUPUNGUZA NAFASI ZA KUPATA CANCER





Kama wewe ni mpenzi wa kutazama habari zinazojiri kila siku, unaweza ukasikia leo usiku kwenye ITV kwamba samaki anafaa kwa afya yako, kesho katika TBC utasikia samaki hafai katika kuishi kwako na utajiuliza mbona wanatuchanganya. Hapana, hakuna anayekuchanganya ila tu dunia inabadilika. Cancer au Saratani ni aina ya maradhi yanayosababishwa na kasoro ya ugawanyikaji wa seli mwilini kama vile uvimbe au vidonda. 


Uchunguzi umefanyika kutoka vyanzo na rejeo zaidi ya 7,000 ukipewa kipaumbele na Food and Agriculture Organization of United Nations (FAGUN) and World Health Organization (WHO) kuandaa kitabu cha kurasa 517. The Food, Nutrition, Physical Activity and Prevention of Cancer: A Global Perspective kimeandikwa na wanasayansi 21 chini ya World Cancer Research Fund and The American Institute of Cancer Research. 


1st Publication ilitolewa mwaka 1997 na Dr. Garl Harrison akiwa kama Mchunguzi wa UCLA na member wa Institute of Medicine wakikita toleo lao la pili The Bible of Nutrition and Cancer.

 Vyanzo vingine navyo vimeonekana kuungana na machapisho haya mawili lakini vikiongezea kuwa Wagonjwa wengi wanaopatwa na kansa au saratani, hupatwa na tatizo hili kutokana na jinsi wanavyoishi huku duniani. 


Hakuna hitaji la kuwa na mshangao kwa kinachojiri kila unapotazama habari usiku. Hivyo njia zifuatazo zinaweza kukusaidia kujiepusha kupatwa na Saratani nazo nyingi huhitaji mabadiliko ya Lifestyle yako wewe mwenyewe.


1. Achana na matumizi ya Tumbaku.


Kulingana na Hospitali ya Muhimbili iliyopo Dar es Saalam, watu zaidi ya 32 wanaoenda kupewa tiba kila mwaka huwa na ugonjwa wa Saratani ya mapafu. Tumbaku ni mmea unaotoa majani ambayo hukaushwa na hutumika kutengenezea sigara.

Sana sana, kwa sababu tumbaku hutumika katika sigara na ndicho wanachopendea wavutaji, huwasababishia aina tofauti za saratani ambazo ni Saratani katika Ini, Kinywa, Koo, Larynx (zoloto, mwanzo wa koromeo unaohusika na kutoa sauti), Pancreas, Kibofu na Figo. Cervix (mlango mwembamba wa uzazi unaoungana na uke) na Oral cavity (mdomo) husababishwa na Xhewing Tobacco.



NB: Kwa upande wa pili, moshi kutoka kwenye magari na mashine zingine  huweza kusababisha Kansa ya Mapafu.

Ukiacha kuvuta sigara na ukajitahidi kujiweka mbali na moshi kutoka viwandani unaweza kuepusha kansa ya sehemu za mwili zilizotajwa hapo juu. Jinsi ya kuachana na uvutaji wa sigara na tumbaku tazama Jinsi ya Kuachana na Tabia sugu uliyonayo.



2.  Kula lishe bora ya Afya/A Healthy Balanced Diet.

Ili kupata lishe bora(Balanced diet), ni vyema kama ungejitahidi kuitafuta nahuwa inapatikana kiurahisi hata kama sio kwa asilimia mia moja lakini asilimia tisini na tano inachukua hitaji kamili kuitwa lishe iliyokamilika. Ili uwezekupata lishe bora jitahidi kufanya vifuatavyo;



    i.    Kula matunda ya kutosha nay a aina tofauti na mboga za majani. Imegundulika kwamba, ulaji wa matunda na vyakula vinavyoujenga mwili kama Maharage, nafaka na mboga za majani husaidia mwili wako kupunguza nafasi za kuangukiwa na Kansa. Chukua nukuu kwamba unalohitaji la kwenda kuangaliwa kama una ulcers ili ujue unahitaji kula aina gani ya maharage au vyakula gani visivyo na gesi za kutibua ulcers.


Jitahidi kujiepusha na unene wa kupindukia kwa kuchagua vyakula vyenye calories kubwa kama sukari iliyosafishwa(refined sugars) na vyakula vyenye mafuta kutoka kwa wanyama.



       ii.   Punguza unywaji wa pombe na vilevi. Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuepusha Saratani ya Matiti, Mapafu, Figo na Ini.

Pia saratani hizi zinaweza kutokea kutokana kiwango unachotumia cha unywaji na pia muda uliotumia kwa kunywa(i.e. kipindi kizima tokea uanze kunywa vilevi).



   iii. Jitahidi kujiwekea mipaka ya kula nyama. Za kutengenezwa. Kulingana na utafiti uliofanywa na International Agency for Research on Cancer, walifikia hitimisho kwamba ulaji mkubwa wa nyama za kutengenezwa huweza kusababisha ongezeko la nafasi ya wewe kupata kansa/saratani.


Ushauri;

    Mafuta ya Mzaituni (Extra Virgin Olive Oil) na Karanga za aina tofauti huweza kupunguza kupata Saratani ya Matiti kwa wanawake.


    Lishe ya Mediterani (Mediterranean diet) huwa sana katika upande wa vyakula vya kijani (Plant based foods and fruits-matunda) nafaka kamili, jamii kunde (Legumes) na nuts (njugu, lozi, korosho)


NB: Watu wanaokula lishe ya Mediterani (Mediterranean diet), kwa kawaida huchagua mafuta ya afya(healthy fats) kama Olive Oil, Siagi na Samaki badala ya Red meat. Ukitaka kujua zaidi juu ya Lishe ya Mediterrani tazama Jinsi ya kupata Lishe ya Mediterrani.


3.  Fanya mazoezi kupata uzito wa kiafya na zoea mazoezi.


Imejulikana kwamba mazoezi yamewapelekea watu wengi kuwa na nguvu kubwa ya mwili kupingana na maradhi tofauti lakini tatizo linakja kwamba wengi wetu wanadamu ni wavivu wa mazoezi na ni kwa sababu wengi hukosa nafasi wakibanwa na kazi zinazowahitaji kukaa ofisini masaa zaidi ya kumi na mbili(12).


Kufanya mazoezi kunaweza basi kupunguza aina fulani za saratani kama ya Matiti, Prostate (tezi ya kiume isaidiayo kuunda manii), Mapafu, Saratani ya Utumbo mpana na Figo.

Jitengenzee ratiba nzuri ya kukufanya uwe na huo wakati wa kufanya mazoezi ya aina yoyote.



4.  Jilinde mbali na mwanga mkali wa jua.

Kujilinda na mwanga mkali wa jua kunakuepusha na kupatwa na UV (Ultra-Violet) Light Rays (Mionzi mikali ya jua) ambayo hushindikana kuzuiwa na Ozone Layer-Ozoni) na kutufikia sisi huku chini. Mionzi hii hupelekea kupata  Saratani ya Ngozi na magonjwa ya macho kama kutokuona vizuri kwa sababu ya mwanga mkali.


Pendelea kukaa kwenye kivuli na pia kama ni vigumu basi vaa hata miwani ya jua (sunglasses)


i      Jiepushe mara kwa mara na jua la mchana ambalo ndilo mara kwa mara hubeba mionzi hii kwa kuvaa nguo zinazokwepa ngozi kuguswa na mionzi hii.



5.  Jitahidi kupata kinga mara kwa mara (get immunized)

Kujaribu kuzuia Cancer kunasaidia pia kupata kinga dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi kama vile;


i. Hepatitis B: Ugonjwa huu huongeza nafasi ya kupatwa na Saratani ya Ini. Chanjo ya ugonjwa huu zimeshauriwa kwa,
Watu wazima ambao hupendelea kufnaya ngono (Sexually active adults) ambao wanayo nafasi kubwa kupataMagonjwa ya zinaa
Watumiaji wazoefu wa madawa ya kawaida nay a kulevya
Wanaume wanaopenda ngono na wanawake wengi
Watu wasiofanya usafi makini wa sehemu zao za siri(pubic areas)
Wanaofanya kazi za kuokoa watu wanahatari ya kushikana na damu chafu au vimiminika vya mndani ya mwili.

ii. Human Popillomavirus(HPV): Huu ni uganjwa wa virusi ambao huweza kusababisha magonjwa mengine kama cervical disease(ugonjwa wa mlango wa uzazi uunganishao uke) na pia Squamous cell cancer(cancer ya ndani ya kichwa na shingo).
Chanjo yake hushauriwa kwa wasichana na wavulana wa miaka 11 hadi 12. Pia ipo chanjo ya vijana(wa kiume na kike) wa miaka 26 au chini yake katika mahospitali tofauti .



6.  Jiepishe na tabia zisizofaa.

Kuna tabia zisizoshauriwa katika jamii ili kujiepusha na maradhi tofauti yanayoweza kumpata mtu. Kizuri zaidi ni kwamba kwa asilimia kubwa kuna njia za kujiepusha na maradhi hayo.

Fanya ngono salama.

- Punguza idadi ya watu unaofanya nao tendo hilo.

- Tumia kondomu

- Watu wenye UKIMWI wanayohatari ya kupata Saratani ya Utumbo mpana na Saratani ya Ini.

-HPV mara kwa mara huambatana na Cervical cancer lakini pia inaweza ikachangia kupata saratani ya Anus (sehemu ya kutolea kinyesi), koo, Uume, na saratani ya uke.

Usichangie vitu vyenye ncha kali.
Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama nyembe au sindano na muathirika wa madawa hupelekea kuambukizwa ugonjwa wa UKIMWI na pia Hepatitis B na C huleta saratani ya Ini. Ukitaka uachane na uvutaji wa madawa ya kulevya tafuta usaidizi wa Madaktari.



7.  Jizoeshe kwenda kupata Body check up mara kwa mara.

Hii hukusaidia wewe kupata kujua ni magonjwa gani yamezuka ndani ya mwili wako na kukupa matumaini ya yale magonjwa ambayo mwili wako unaenda kupona.


Ni wazi kwamba mpaka sasa ninaouhakika kwamba kama hutakuwa mvivu kuzingatia kati ya haya machache niliyokuwekea mbele yako, basi na wewe utakuwa shahidi mwingine wa kuwasaidia wale watakaohitaji kuwa kama wewe usiye umwa na cancer. Jilinde, Jitunze, Isaidie Jamii!


Comments